S.L.P. 580, Mbozi, Songwe, Tanzania

Habari za DiA's

Kujenga nyumba ya kazi yetu: ofisi ya DiA's

Na DiA's · 20 Oktoba 2026 · dakika 1 kusoma

Jessey Kimei akikagua kazi ya ufundi chuma kwa ajili ya ofisi

Mwanzilishi, Jessey Kimei, alikagua kazi ya ufundi chuma kwa ajili ya ofisi ya DiA's huko Ilonga Mahenje, mahali ambapo shughuli za CASA na COPE zitaratibiwa.

Ofisi ya DiA's iko Ilonga Mahenje, Mbozi, mita 230 kutoka barabara kuu ya Tunduma–Dar es Salaam. Ndipo shughuli za CASA na COPE Club zitakaporatibiwa: mikutano, kumbukumbu za michango, mafunzo ya Prefects, na kuwapokea wanaohitaji msaada.

Ukaguzi wa kazi

Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu, Jessey Kimei, alitembelea karakana kukagua kazi ya ufundi chuma inayoandaliwa kwa ajili ya ofisi. Lengo ni kuhakikisha kila hatua ya ujenzi inafanyika kwa ubora na kwa matumizi sahihi ya rasilimali.

Kinachohitajika bado

Ofisi bado inahitaji vifaa vya umaliziaji, vikiwemo wall gypsum putty kwa kusawazisha kuta, gypsum board kwa dari, na plywood board kwa meza za ofisi. Kila mchango, mkubwa au mdogo, unatusogeza karibu na ofisi itakayowahudumia wanajamii wengi zaidi.

Ukipenda kuchangia, tazama ukurasa wa Changia. Kumbukumbu za michango yote hutunzwa, na taarifa ya matumizi hutolewa kwa wachangiaji.

Shiriki makala hii:

← Rudi kwenye Blog